Jumamosi 28 Novemba 2026 - 08:40
Husseiniya ya Imaam Mahdi Tabora Yaadhimisha Mazazi ya Bibi Fatima Zaharaa (as), Waumini Wakumbushwa Kuiga Mwenendo Wake

Hawza/ Husseiniya ya Imamul Mahdy (as), iliyopo mkoani Tabora, imefanya majlis maalumu ya kuadhimisha kumbukumbu ya mazazi ya Bibi mtukufu Sayyidat Fatima Zaharaa (as), binti mpendwa wa Mtume Muhammad (saww).

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Majlis hiyo iilifanyika siku ya Alhamisi, Novemba 26, 2026, baada ya Swala ya Maghrib, ikiwa na lengo la kuenzi maisha matukufu ya Bibi Fatima Zaharaa (as), pamoja na kuimarisha uelewa wa waumini kuhusu nafasi yake na mafundisho yake katika Uislamu.

Katika majlis hiyo, waumini walipata fursa ya kukumbushwa utukufu na nafasi ya Bibi Fatima Zaharaa (as), ambaye maisha yake ni mfano bora wa kuigwa katika ibada, uchamungu, subira, kujitolea, malezi bora na kuzingatia maadili mema.

Aidha, majlis hiyo ilikuwa ni fursa ya kuhamasisha waumini, hususan wanawake na vijana, kujifunza kutokana na mwenendo na mafundisho ya Bibi Fatima Zaharaa (as), na kuyatekeleza katika maisha yao ya kila siku.

Kwa upande mwingine, waandaaji wa majlis hiyo wamemshukuru Mwenyezi Mungu (swt) kwa kufanikisha shughuli hiyo, huku wakiwaombea kheri na malipo mema waumini wote waliochangia, kushiriki katika maandalizi na kuhudhuria majlis hiyo.

Majlis hiyo ilihitimishwa kwa dua ya kumuomba Mwenyezi Mungu (swt) ayakubali matendo mema ya waumini na awawezeshe kuishi kwa kufuata mafundisho matukufu ya Ahlul Bayt (as).

Husseiniya ya Imaam Mahdi Tabora Yaadhimisha Mazazi ya Bibi Fatima Zaharaa (as), Waumini Wakumbushwa Kuiga Mwenendo Wake

Husseiniya ya Imaam Mahdi Tabora Yaadhimisha Mazazi ya Bibi Fatima Zaharaa (as), Waumini Wakumbushwa Kuiga Mwenendo Wake

Husseiniya ya Imaam Mahdi Tabora Yaadhimisha Mazazi ya Bibi Fatima Zaharaa (as), Waumini Wakumbushwa Kuiga Mwenendo Wake

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha